Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kuutazama Ulimwengu

Kuutazama Ulimwengu

UJERUMANI

Katika mwaka wa 2012, mahakama moja kuu nchini Ujerumani iliamua kwamba mtu hawezi kuacha kirasmi kanisa ambalo limeandikishwa kuwa shirika la umma na bado aendelee kuwa mshiriki wa kanisa hilo. Wakatoliki wanaoacha rasmi kuwa washiriki wa kanisa, na hivyo kuacha kulipa kodi ya kanisa, lakini bado wanaendelea kwenda kanisani, huenda wakazuiwa kula Sakaramenti, kuungama, kupata vyeo kanisani, na hata huenda wasizikwe na kanisa.

ULIMWENGU

Uchunguzi uliofanywa kuhusu dini unaonyesha kwamba watu wanaodai “kutojihusisha na dini yoyote” ingawa si lazima wawe wanaamini kwamba hakuna Mungu, sasa wanafikia bilioni 1.1. Wao wanashika nafasi ya tatu, wakitanguliwa na Wakristo ambao ni bilioni 2.2 na Waislamu ambao ni bilioni 1.6. Wahindu wanashika nafasi ya nne wakiwa bilioni 1 hivi.

JAPANI

Wanasayansi nchini Japani wamegundua kwamba “kusifiwa huchochea sehemu za ubongo zinazohusiana na kupokea zawadi,” na hivyo kutokeza “hisia ya furaha.” Inaonekana utafiti huo unaunga mkono wazo la kwamba kumsifu mtu ni njia nzuri ya kumchochea afanye vizuri zaidi.

BOLIVIA

Mwishoni mwa mwaka wa 2012, Bolivia ilifanya sensa ya nchi nzima. Ili hesabu ya watu iwe sahihi, wakazi wa Bolivia walipaswa kubaki nyumbani siku hiyo. Isitoshe, watu hawakuruhusiwa kuendesha magari ya kibinafsi, mipaka ilifungwa, na utumiaji wa kileo ulipigwa marufuku.

ITALIA

Katika uchunguzi mmoja, Waitalia walisema kwamba wao hucheza na watoto wao kwa wastani wa dakika 15 kwa siku. “Ni mzazi mmoja tu kati ya watano anayefikiri kwamba michezo hiyo inaelimisha,” linasema gazeti La Repubblica. Mbuni wa michezo inayochezwa juu ya ubao, Andrea Angiolino, anasema kwamba kupitia michezo, wazazi husaidia watoto wao kukuza uwezo wao wa kubuni na pia wanajifunza “kufuata sheria.”