WIMBO NA. 137
Wanawake Waaminifu, Dada Wakristo
-
1. Sara, Maria, Ruthu na wengine—
Washikamanifu, wenye uwezo.
Waliomwogopa Yehova Mungu.
Na majina yao tunayajua.
Kuna wengi kama hao pia,
Waliokuwa na imani kwa Mungu.
-
2. Wema na fadhili na ujasiri;
Wengi huvutiwa na sifa hizo.
Wanawake hao twawakumbuka,
Ambao ni vielelezo bora.
Kama hao, dada zetu pia,
Mwastahili sana pongezi na sifa.
-
3. Mama, mabinti, wake, na wajane,
Mnaotimiza mengi kwa shangwe.
Wenye kiasi na ujitiisho,
Mungu awapenda, jipeni moyo.
Yehova na awategemeze.
Dumuni imara, mtapata tuzo.
(Ona pia Flp. 4:3; 1 Tim. 2:9, 10; 1 Pet. 3:4, 5.)