Awamu ya 3 ya Picha za Uingereza (Septemba 2016 Hadi Februari 2017)
Ona kazi iliyofanywa katika ofisi mpya ya tawi ya Mashahidi wa Yehova nchini Uingereza kati ya Septemba 2016 na Februari 2017.
Septemba 13, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Kifaa cha kuchimba ardhi kinapakia mchanga kwenye lori. Mchanga uliochimbuliwa utahamishiwa sehemu nyingine ili kutayarisha eneo kwa ajili ya ujenzi.
Septemba 15, 2016—Eneo la kutegemeza ujenzi
Wajitoleaji wa Idara ya Umeme wanafunga nyaya. Jengo hili litakuwa na ofisi za muda na chumba cha kulia chakula ambavyo vitatumika wakati wa ujenzi wa ofisi mpya ya tawi iliyo karibu.
Septemba 19, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Picha ya angani inayoonyesha barabara ya kuingia kwenye ofisi ya tawi. Upande wa kushoto, matayarisho yanafanywa ya kutengeneza bustani, kidimbwi, na eneo litakalowawezesha watu kuona maeneo mengine kwa ajili ya wenyeji na wageni.
Novemba 3, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Zege kutoka eneo hilo zinapondwa-pondwa na kutumiwa tena kwa ajili ya kutengeneza barabara za ofisi hiyo.
Novemba 4, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Sehemu ya mbele, wafanyakazi wanajenga barabara za muda na za kudumu. Wanatumia kitu fulani kinachosawazisha sehemu ya chini ya barabara. Upande wa kulia nyuma ya picha, kifaa cha kukandamiza sehemu ya chini kabla ya kuweka kitu hicho.
Novemba 5, 2016—Tukio la kuhamisha ofisi ya tawi
Wajitoleaji wapata habari katika mojawapo ya matukio 18 yaliyopangwa kotekote nchini Uingereza na Ireland na Halmashauri ya Mradi wa Ujenzi. Mashahidi zaidi ya 15,000 walihudhuria matukio hayo, na wengi wao walijitolea kushiriki katika mradi wa ujenzi.
Novemba 28, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Wafanyakazi wakiweka samadi kwenye mti ambao unamea vizuri ukipandwa karibu na maeneo yenye maji. Mti huu ni mojawapo ya miti 700 iliyopandwa katika eneo hili. Bwawa limetengenezwa ili kupunguza mafuriko wakati wa mvua kubwa, ili kuhifadhi maji ya mvua, na kisha kuyaondoa katika eneo hilo hatua kwa hatua.
Desemba 5, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Siku yenye mawingu, kazi ya kuhamisha mchanga inaongezeka kadiri kazi inavyofikia hatua ya mwisho. Ardhi yenye ukubwa wa mita 160,000 za mraba—inatosha kujaza lori hizi 10,000!
Desemba 6, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Timu ya kutandaza ardhi inatayarisha udongo wa kupanda mimea kwa ajili ya uzio kwenye mpaka wa bustani. Bustani hii na eneo linalozunguka lina aina 11 ya miti na aina 16 ya mimea.
Desemba 19, 2016—Majengo ya makazi
Upande wa kushoto, trekta inachimba shimo kwa ajili ya msingi. Kwanza, kifaa kinachimba shimo. Kisha, zege inapitishwa kwenye kifaa hicho wakati kinapotolewa. Mwishowe, kama inavyoonekana katika sehemu ya kati ya picha, wachimbuzi wanaingiza chuma kwenye zege hiyo ili kukamilisha msingi. Sehemu zaidi ya 360 zimetengenezwa hivyo ili kuwa sehemu ya msingi wa majengo ya makazi.
Desemba 29, 2016—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Asubuhi yenye baridi, fundi bomba anaunganisha bomba la maji ambalo litatumiwa katika ofisi za muda.
Januari 16, 2017—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Trekta inaondoa mchanga na uchafu uliojikusanya kwenye bwawa lililoko mwishoni mwa eneo la ujenzi. Mabwawa kadhaa yalikuwa katika hali mbaya na yalihitaji kurekebishwa. Mabadiliko katika ujenzi utasaidia vidimbwi hivyo visipatwe na mmomonyoko wa udongo na visifurike maji. Samaki zaidi ya 2,500 walihamishwa kwa uangalifu na kupelekwa kwenye mabwawa mengine kabla ya ukarabati kuanza.
Januari 17, 2017—Makazi
Picha ya angani kutoka upande wa kushoto. Upande wa mbele, kazi ya kuweka msingi wa majengo mawili ya makazi imeanza. Upande wa chini kulia, sehemu za msingi zinaonekana. Upande wa chini kushoto, matayarisho yamefanywa kwa ajili ya kuweka msingi. Sehemu ya katikati, trekta inaendelea kuchimba misingi.
Januari 23, 2017—Eneo la kutegemeza ujenzi
Mjitoleaji anayeshirikiana na kikundi cha kumalizia ujenzi anatumia silicon kwenye mlango ili kujitayarisha kwa ajili ya kupaka rangi. Wageni wataweza kuona onyesho la mambo yaliyohusika katika ujenzi na jinsi unavyoendelea na wataona maendeleo ya kazi kutoka sehemu ya juu.
Februari 14, 2017—Makazi
Kifaa kinachowezesha mashine kuzunguka inaingizwa mahali pake. Mashine hiyo yenye urefu wa mita 40, inaweza kuinua uzito wa hadi tani 18
Februari 15, 2017—Makazi
Vyuma vilivyokorogewa kwa zege vinahakikisha uimara. Chuma zilizo katikati zitatumiwa kuunganisha sehemu nyingine.
Februari 17, 2017—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Mafundi wa umeme wakiweza bango la JW.ORG kwenye ukuta ulio kwenye mwingilio wa ofisi ya tawi.
Februari 17, 2017—Eneo la ujenzi wa ofisi ya tawi
Picha ya angani ya barabara kwenye eneo la kuingilia. Upande wa kushoto juu, mabango mapya ya JW.ORG yanaonyesha ofisi ya tawi. Kidimbwi na bustani itaongeza umaridadi wa sehemu ya kuingilia.
Februari 24, 2017—Makazi
Mashine hii inafanya kazi kwenye eneo lenye upana wa majengo manne kati ya majengo matano ya makazi. Sehemu ya mbele ya picha, wafanyakazi wanatayarisha zege kwa ajili ya maegesho ya magari katika sehemu ya chini ya jengo moja la makazi. Chuma imara ziko tayari kutumiwa kwa ajili ya kuta za jengo hilo.